
Aliekua meneja wa klabu ya Chelsea Jose Mourinho amemtaka meneja wa sasa wa klabu hiyo Carlo Ancelotti kutambua dhoruba la kutokua na wachezaji wake muhimu sio miujiza bali hata yeye alipokua madarakani huko Stamford Bridge liliwahi kumpata.
Mourinho ambe kwa sasa anakinoa kikosi cha klabu ya Real Madrid ya nchini Hispania amesema Carlio Ancelotti anatakiwa kutambua na kuikubali changamoto hiyo ambayo amedai haiweze kuzuilika kutokana na mazingira ya soka yaliyopo.
Amesema katika msimu wa mwaka 2006-07 akiwa na klabu ya Chelsea aliouona msimu huo mchungu kwake kutokana na kuwapoteza kwa pamoja wachezaji wake muhimu kama John Terry, Frank Lampard pamoja na Ricaldo Cavalho ambao walikua majeruhi huku uwezo wa mshambuliaji wake Didier Drobga ulikua dhaifu na alikubaliana na matokeo yaliyopatikana.
Mourinho ametoa mfano huo baada ya meneja wa sasa wa klabu ya Chelsea Carlo Anceloti kupoteza muelekeo ndani ya kikosi chake ambacho kilikuta kikifungwa michezo miwili mfululizo huku sababu ikionekana ni kufuatia kukosekana kwa baadhi ya wachezaji wake muhimu.
Hata hivyo amemtaka Carlo kua mtulivu na kukubaliana na mazingira yaliyopo katika kikosi chake ambayo pia msimu huu yalijitokeza kwa mashetani wekundu ambao kwa kipindi kirefu walicheza bila ya kuwa na beki wao Rio Ferdnand pamoja na mshambuliaji Wayne Rooney.
Mourinho pia akazungumzia ushindani uliopo kwenye nafasi za juu za ligi kuu ya soka nchini Uingereza kupitia mfano wa kikosi cha Arsenal ambacho kimeshindwa kufikia malengo la kuongoza ligi hiyo baada ya kupoteza mchezo wa mwishoni mwa juma lililopita.
Amesema kikosi cha klabu hiyo kwa ujumla ni kizuri na kina uwezo wa kufanya lolote kinapokutana na vikosi vingine, lakini udhaifu wake ni kukubali kufungwa na yoyote yule tena katika michezo muhimu ambapo ametolea mfano michezo ambayo ilishuhudia The Gunners wakipoteza nyumbani dhidi ya Newcastle Utd pamoja na Spurs.
Wakati Mourinho akiizungumzia Arsenal kwa namna hiyo, Arsene Wenger ambae ni meneja wa klabu hiyo ya jijini London amesema amejitoa muhanga kwa hali na mali katika kuhakikisha wachezaji wake wanafanya vyema lakini kubwa alilolibaini ni kuridhika mapema kwa kikosi chake hali ambayo imekua ikiwagharimu kwa kiasi kikubwa mara kwa mara.
Akitolea mfano wa mchezo wa mwishoni mwa juma lililopita mzee huyo wa kifaransa amesema kulikua hakuna sababu ya wachezaji wake kuridhishwa na hatua ya kuongoza kwa idadi ya mabao mawili waliyoyapata katika kipindi cha kwanza bali walistahili kuendelea kucheza kwa kujituma lakini udhaifu waliouonyesha uliwagharimu na kujikuta wakitoa nafasi kwa wapinzani wao kusawazisha na kuongeza bao la ushindi.
No comments:
Post a Comment