
Meneja wa klabu ya Chelsea Carlo Ancelotti ameendelea kuwatoa hofu mashabiki wa klabu hiyo baada ya kuthibitisha ataendelea kuwepo licha ya taarifa kuzagaa huenda akaondoka.
Carlo Ancelotti ambae amedai hashirikishi katika maamuzi yanayofanywa huko Stamfode Bridge amesema taarifa zozote zinazendelea kutolewa dhidi yake si za kweli na hadhani kama ataondoka leo ama kesho.
Amesema anauheshimu mkataba wake aliosaini na uongozi wa klabu ya Chelsea ambao unafikia kikomo mwaka 2012 hivyo ni jukumu lake kuhakikisha anatimiza malengo aliyokubaliana na uongozi wa klabu hiyo na si kuachia njiani.
Meneja huyo wa kimaaifa toka nchini Italia mwishoni mwa juma hili alikaririwa na vyombo vya habari akisema kuwa amechoshwa na utaratibu wa uongozi wa klabu ya Chelsea ambao umekua haufanyi maamuzi ya kumshirikisha ambapo aligusia suala la kuondolewa kwa msaidizi wake Ray Wilkins na kuteuliwa kwa msaidizi mwingine.
No comments:
Post a Comment