KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, November 19, 2010

FA WAILIPA LIVERPOOL, ARSENAL PAMOJA NA SPURS.


Baada ya kutakiwa kuingilia kati suala la matibabu ya wachezaji wanapoumia wakiwa kwenye michezo ya kimataifa ya kirafiki, uongozi wa chama cha soka nchini Uingereza FA umetangaza kuilipa klabu ya Liverpool kiasi cha fedha ambazo zitatumika kwenye harakati za matibabu ya nahodha na kiungo wa klabu hiyo Steven Gerrard ambae alimaliza mchezo wa juzi akiwa na maumivu ya nyonga.

FA wametimiza sharti hilo ikiwa ni siku moja tu baada ya uongozi wa klabu ya Liverpool pamoja na meneja wa klabu ya Stoke City Tony Pulis kuonyesha kuchukizwa na kitendo cha kiungo huyo kuumia akiwa na timu ya taifa na gharama za matibabu yake zilitegemewa huenda zingetolewa na klabu ya Liverpool.

Kufuatia suala hilo uongozi wa klabu ya Liverpool umepewa kiasi cha paund laki tano ambazo zitatumika kama gharama za kumtibu Steven Gerrard ambae anatarajia kuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha majuma manne yajayo.

Hata hivyo imeelezwa kuwa malipo hayo ya fedha hizo yanadaiwa kutolewa na kampuni ya bima iliyoingia mkataba na chama cha soka nchini Uingereza ambacho pia kimelazimika kuilipa klabu ya Arsenal pamoja na klabu ya Tottenham.

Arsenal wamelipwa fedha hizo kufuatia kuumia kwa winga wao Theo Wallcot huku Tottenham Hotspurs wakilipwa kufuatia kuumia kwa Jamaine Defoe ambao wote kwa pamoja waliumia wakiwa kwenye utetezi wa taifa la Uingereza.

No comments:

Post a Comment