
Mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Uingereza na klabu ya Man Utd Wayne Rooney huenda akarejea tena uwanjani kesho kwenye mchezo wa ligi kuu nchini humo ambapo Mashetani wekundu watakua nyumbani wakiwakaribisha Wigan toka DW Stadium.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25 ambae hajaonekana uwanjani tangu Oktoba 16 mwaka huu anatarajiwa kuonekana tena uwanjani baada ya kurejea nchini Uingereza akitokea nchini Marekani alipokwenda kufanyiwa matibabu pamoja na mazoezi maalum.
Taarifa za kurejea tena uwanjani kwa mshambuliaji huyo zimethibitishwa na meneja wa klabu ya Man Utd Sir Alex Ferguson alie safari kutoka nchini Qatar kurejea nchini Uingereza kuuwahi mpambano wa kesho ambao utapigwa huko old Trafford.
Akizungumza na waandishi wa habari nchini Qatar kabla ya safari yake ya kurejea nchini Uingereza meneja huyo mwenye umri wa miaka 68 amesema mshambuliaji huyo hali yake imerejea kama ilivyokua zamani na ana matumaini makubwa ya kumtumia kwenye mchezo wa kesho ambao watakuwa na kazi nzito ya kusaka point tatu muhimu kwa lengo la kuondokana na matokeo ya sare yaliyowaandama juma lililopita.
Amesema mbali na kutarajia kumchezesha hiyo kesho pia ana matumaini makubwa ya kumuanzisha kwenye kikosi cha kwanza cha klabu ya Man Utd itakachoshuka ndimbani siku ya jumatano katika mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Rangers watakaokuwa nyumbani huko nchini Scotland.
Katika hatua nyingine waandishi wa habari waliokua kwenye mkutano huo walimuuliza Sir Alex Ferguson mustakabali wake wa kustahaafu kufundisha soka ndani ya klabu ya Man Utd hatua ambayo kila leo amekua akiiahirisha kwa sababu za muda wake wa kufanya hivyo kutokua tayari.
Sir Alex Ferguson amejibu swali hilo kwa kusema kwamba anachofahamu yeye hatua ya kustahaafu huwa inafikiwa na vijana kwa sababu huwa wana nafasi nyingine ya kufanya kitu mbadala na si kwa wazee ambao huwa hawana cha kufanya mara baada ya kufikia maamuzi hayo.
No comments:
Post a Comment