
Shirikisho la soka duniani FIFA limetoa angalizo kwa wajumbe wake wanaotarajiwa kupiga kura ya kuchagua nchi zitakazoandaa fainali za kombe la dunia za mwaka 2018 pamoja na 2022.
Angalizo hilo kwa wajumbe ni kuhakikisha wanachagua nchi kutokana na vigezo maalum vilivyowekwa kwa lengo la kuziwezesha fainali za kombe la dunia kutokua na mapungufu makubwa zitakapokua zikichezwa katika nchi watakazozichagua kwa mwaka 2018 pamoja na 2022.
Kamati kuu ya FIFA tayari imeshatembelea katika nchi zinazoomba nafasi ya kuandaa fainali za kombe la dunia kwa miaka hiyo na kubaini mapungufu kadhaa ambayo yametakiwa kuangaliwa vyema na wajumbe kabla ya kuamua kutoa kura zao kwa nchi Fulani ambayo wanaona inafaa kuandaa fainali hizo.
Mapungufu yalioonekana katika nchi ya Uingereza inayoomba nafasi hiyo ni upungufu wa hoteli zenye hadhi ya nyota tano pamoja na viwanja vichache vya kufanyia mazoezi kwa timu shiriki.
Nchi za Hispania na Ureno zilizoomba kuandaa fainali hizo kwa pamoja huku nchi ya Uholanzi ikishirikiana na Ubelgiji zimeonekana kuwa na mapungufu pia.
Mapungufu kwa nchi hizo zilizoomba kuandaa kwa pamoja ni kuhusu vifaa na umbali wa baadhi ya viwanja huku nchini Urusi ikiendelea kujinadi kujenga viwanja vingi zaidi ambavyo vitagharimu mabilion ya dola za kimarekani.
Katika fainali za mwaka 2022 mataifa ya barani Asia yanapewa nafasi kubwa ya kushinda huku nchi ya Qatar ikishauriwa kutafuta miundo mbinu ya kupunguza joto la kupinduikia ambalo huenda likawa karaha kwa mataifa shiriki na mashabiki wake watakapoelekea nchini humo endapo watafanikiwa kuipata nafasi ya kuandaa.
Hata hivyo tayari serikali ya nchi hiyo imejinadi kusaka namna ya kubuni miundo mbinu hiyo ambayo wana uhakika itawawezesha kuwa na kigezo muhimu cha kuipata nafasi ya kuandaa fainali za kombe la dunia kiurahisi.
Nchi nyingine za bara la Asia zilizoomba kuandaa fainali hizo kwa mwaka 2011 ni Australia, Korea Kusini pamoja na Japan.
Nchi ya Marekani ambayo iliomba nafasi ya kuandaa kwa mwaka 2022 ilikua ikipewa nafasi kubwa lakini kufuatia serikali ya nchi hiyo kupuuzia maombi yaliyowasilishwa FIFA imelazimika kuenguliwa katika kinyang’anyiro hicho.
No comments:
Post a Comment