
Winga wa kimataifa toka Jamuhuri ya watu wa Korea na klabu ya Bolton Wanderers Lee Chung-yong amekubalia kijitia kitanzi ndani ya klabu hiyo hadi mwaka 2013.
Lee Chung-yong amekubalia kijivika kitanzi hicho baada ya kusaini mkataba wa miaka mitatu kufuatia mkataba wake wa sasa kutarajia kufikia kikomo mwishoni mwa msimu huu.
Sababu kubwa ya winga huyo kukubali kusalia klabuni hapo ni kufutia mipango mizuri aliyoongea na meneja wake Owen Coyle aliaonyesha dhamira ya mapinduzi klabuni hapo msimu huu huku kikosi chake kikishika nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi kwa kufikisha point 22.
Owen Coyle amezungumza na vyombo vya habari na kueleza kwamba hatua ya Lee mwenye umri wa miaka, 24 kukubalia kusaini mkataba mpya imemfurahisha na ana imani kubwa baadhi ya malengo yake yatatimia kwa kuendelea kuwa na wachezaji wenye uzoefu kama winga huyo.
Wakati akionyesha furaha ya Lee kusiani mkataba mpya, Owen Coyle pia akazungumzia mkakati wa kuhakikisha anaendelea na wachezaji walio kwenye kikosi chake kwa sasa huku akimgusia mshambuliaji wake wa kimataifa toka nchini Sweden Johan Almander ambae tayari ameshaanza kuhusishwa na taarifa za kutaka kusajiliwa na klabu nyingine itakapofika mwezi Januari mwaka 2011.
Amesema anatambua mshambuliaji huyo msimu huu ameonyesha uwezo mkubwa wa kuisaidia Bolton Wanderers hadi hapa ilipofika hivyo hatokua tayari kumuachia.
No comments:
Post a Comment