
Hatimae mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Uingereza na klabu ya Tottenham Hotspur Jermain Defoe ameanza rasmi mazoezi baada ya kuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha mwezi mmoja kufuatia jeraha la kisigino lililokua likimsumbua.
Defoe mwenye umri wa miaka 28 amerejea mazoezini huku akionekana mwenye hamu ya kutaka kuonyesha uwezo mkubwa atakapopata nafasi ya kujumuishwa kikosini na meneja wake Harry Redknapp.
Kurejea mazoezini kwa Jermain Defoe kumewashangaza wengi kufuatia taarifa zilizotolewa siku za nyumba ambazo zilidai kwamba huenda ingemchukua muda wa miezi mitatu mshambuliaji huyo kupona jeraha lililokua likimkabili toka Septemba 7 aliposhiriki kwenye mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Uswiz.
Hata hivyo kurejea kwake huenda kukawa kumeamsha ari kwa wachezaji wengine klabuni hapo kufuatia hali ya kusuasua iliyojiri ndani ya kikosi cha spurs kwa kipindi cha majuma mawili kablo ya ushindi wa mwishoni mwa juma lililopita kupatikaba mbele ya Blackburn Rovers.
Licha ya mashabiki na wachezaji wa Spurs kufurahishwa na kitendo cha kurejea kwa mshambuliaji huyo, klabu hiyo ya jijini London tayari imeshatangaza kumkosa kwa kipindi cha miezi mitatu ijayo kiungo wa kutumainiwa Tom Huddlestone anaesumbuliwa na maumivu ya kifundo cha mguu.
Meneja msaidizi wa klabu hiyo Kevin Bond amesema, hii leo kiungo huyo alitarajiwa kwenda kumuona mtalaamu kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji, na kwa sasa wanajiandaa kumtumia kiungo Jermaine Jenas kuziba nafasi yake kuanzia mchezo wa mwishoni mwa juma hili ambapo watacheza na mahasimu wao wakubwa Arsenal.
No comments:
Post a Comment