
Kiungo wa klabu ya Arsenal na timu ya taifa ya Ufaransa Samir Nasri amesema anaamini ligi kuu ya soka nchini Uingereza kwa sasa haina kikwazo kufuatia uwiyano wa kipoint kupungua kati ya Chelsea wanaongoza ligi dhidi ya washika bunduki hao walioa katika nafasi ya pili kwa sasa.
Samir Nasri ametoa mtazamo huo huku akifananisha msimu huu na msimu uliopita ambapo klabu hizo mbili ziliachana kwa kiasi kikubwa na kufikia hatua ya klabu ya Chelsea kutwaa ubingwa kwa tofauti ya point 11.
Amesema wengi walidhani Chelsea ilikua kikwazo wakati ilipokua ikiongoza ligi kwa tofauti ya point tano lakini hii leo imejidhihirisha wazi kwamba ubingwa upo wazi kwa klabu yoyote ambayo inawadai point chache mabingwa hao watetezi.
Wakati kiungo huyo wa kifaransa ambae nae yupo na kikosi cha nchi yake kinachoajiandaa na mchezo wa kesho wa kimataifa wa kirafiki, mchezaji wa zamani wa klabu ya Arsenal Andres Limpar ameipa nafasi kubwa klabu hiyo kufanya vyema msimu huu na ikiwezekana kutwaa ubingwa wa soka nchini Uingereza.
Andres Limpar amesema juhudi zilizofanywa na wachezaji wa klabu ya Arsenal za kufikisha point 26 ambazo zinawafanya kuwa katika nafasi ya pili zinamdhihirishia kikosi hicho kitatoa changamoto kubwa kwa mabingwa watetezi.
No comments:
Post a Comment