
Kiungo wa kimataifa toka nchini Uingereza na klabu ya Liverpool Joe Cole anatarajiwa kuwa miongoni mwa wachezaji watakaoshuka ndimbani mwishoni mwa juma hili kuwakabili Spurs watakapokua nyumbani huko jijini London.
Joe Cole anatarajiwa kurejea tena uwanjani baada ya kuwa nje kwa muda wa majuma matatu kufutia maumivu ya nyonga yaliyokua yakimsumbua baada ya kuumia kwenye mchezo dhidi ya Bolton uliomalizika kwa Liverpool kupata ushindi wa bao moja kwa sifuri.
Meneja wa klabu ya Liverpool Roy Hodgson amethibitisha taarifa hizo huku akieleza kwamba kiungo huyo alimtarajia huenda angerejea tena uwanjani mwishoni mwa juma lililopita walipocheza na West Ham Utd lakini taarifa zilizotolewa na daktari zilishauri mchezaji huyo kupumzika kwa muda wa juma moja zaidi.
Roy Hodgson amesema kurejea kwa kiungo Joe Cole mwishoni mwa juma hili anaamini kutaendelea kuamsha ari ya kusaka ushindi katika mchezo dhidi ya Tottenham pamoja na michezo mingine ijayo.
No comments:
Post a Comment