KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, November 22, 2010

NIPO TAYARI KWA EL CLASSICO.


Meneja wa klabu ya Real Madrid Jose Mourinho ameonyesha kuridhishwa na mwenendo wa kikosi chake ambacho mpaka sasa hakijapoteza mchezo hata mmoja kwenye michuano ya ligi kuu ya soka nchini Hispania.

Mourinho ameonyesha kufurahishwa huko, kufuatia matokeo mazuri yanayoendelea kupatikana kila wanapoingia uwanjani hali ambayo amedai inamfariji kila kukicha.

Amesema kikosi chake kina damu changa hatua mbayo anaamini itakmuwezesha kufikia malengo mazuri yaliyowekwa mwishoni mwa msimu huu hasa ukizingatia kwa sasa kikosi hicho kinaongoza ligi ya nchini Hispania kwa kufikisha point 32.

Akizungumzia mchezo ujao wa ligi ambao utamkutanisha na mabingwa watetezi Fc Barcelona Mourinho amesema yu tayari kukimuru kikosi chake kupambana na kuhakikisha wanapata ushindi ambao utawawezesha kuvunja mwiko wa kupoteza point tatu kila wanapocheza na mahasimu hao.

Amesema kwa namna kikosi chake kinavyoendelea kumekuwa na matumaini mazuri na kuzipata point tatu muhimu katika mpambano huo ambao unasubiriwa kwa hamu kubwa nchini Hispania pamoja na ulimwengu.

No comments:

Post a Comment