KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, November 23, 2010

Mike Williamson AFUNGIWA MECHI TATU NA FA.


Baada ya ya kamati ya nidhamu ya chama cha soka nchini Uingereza kukutana jana kujadili tukio lililofanywa na beki wa klabu ya Newcastle Utd Mike Williamson la kumpiga kichwa mshambuliaji wa klabu ya Bolton Wanderers Johan Elmander katika mchezo uliozikutanisha timu hizo mwishoni mwa juma lililopita, kamati hiyo imetoa maamuzi yake.

Kamati hiyo ambayo ilitumia picha za televisheni kuhakikisha tukio hilo, imebaini kuwa beki wa klabu ya Newcastle Utd Mike Williamson alimpiga kichwa kwa makusudi mshambuliaji Johan Elmander hivyo imetangaza kumfungia kutokucheza michezo mitatu.

Taarifa iliyotolewa na chama cha soka nchini uingereza mara baada ya kamati hiyo kukutana na kutoa maamuzi, imeeleza kwamba beki Mike Williamson alistahili kuonyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja mara baada ya kufanya tukio hilo lakini kwa bahati mbaya muamuzi Howard Webb hakuona kitendo hicho hivyo adhabu iliyotolewa instahili.

Hata hivyo chama cha soka nchini Uingereza kimetoa muda kwa beki huyo kukata rufaa kwa siku ya hii leo hadi itakapofika mishale ya saa 12 jioni endapo atakua hajaridhishwa na adhabiu iliyotolewa dhidi yake.

Kwa mantiki hiyo Mike Williamson ataikosa michezo ya klabu yake pale itakapocheza na Chelsea mwishoni mwa juma hili, mchezo wa Disemba 5 ambao utashuhudia West Brom v Newcastle na mchezo wa Disemba 11 ambapo Newcastle v Liverpool.

No comments:

Post a Comment