KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, November 25, 2010

Luis Suarez AFUNGIWA MECHI SABA BAADA YA KUMNG'ATA Otman Bakkal.



Nahodha na mshambuliaji wa klabu ya Ajax Amsterdam ya nchini Uholanzi Luis Suarez amefungiwa kutokucheza michezo saba ya ligi nchini humo baada ya kubainika alimng’ata kiungo wa klabu ya PSV Eindhoven Otman Bakkal pale timu hizo zilipokutana mwishoni mwa juma lililopita.

Luis Suarez amefungiwa kutokucheza michezo hiyo kufuatia uthibitisho uliopatikana kupitia picha za televisheni ambazo zinaonyesha, mshambuliaji huyo alimng’ata Otman Bakkal sehemu za bega la mkono wa kushoto baada ya kuibuka malumbano kati ya wachezaji wa klabu hizo pinzani nchini Uholanzi.

Malumbano kati ya wachezaji hao yaliibuka baada ya muamuzi Bjorn Kuipers kumuonyesha kadi nyekundu ya moja kwa moja Rasmus Lindgren wa Ajax kufuatia kumchezea rafu kiungo wa Ibrahim Afellay wa PSV Eindhoven.

Muamuzi Bjorn Kuipers hakufanikiwa kukiona kitendo kilichofanya na Suarez cha kumng’ata Otman Bakkal kutokana na kuwa katika harakati za kutuliza zogo lililoibuka.

Kufungiwa kwa mshambuliaji huyo ambae anakumbukwa na wengi kufuatia kuushika mpira uliokua unaelekea nyavuni kwenye mchezo wa hatua ya robo fainali ya kombe la dunia dhidi ya Ghana, kunampa nafasi ya kurejea tena uwanjani kucheza michezo ya ligi Februari 4 mwaka 2011.

Hata hivyo kufungo hicho hakiingiliani na michezo ya ligi ya mabingwa barani Ulaya ambapo majuma mawili yajayo Ajax watarejea tena uwanjani kumalizia mchezo wa hatua ya makundi kwa kucheza na AC Milan huko Sun Siri nchini Italia na Louis Suarez atakuwepo kikosini.

No comments:

Post a Comment