
Meneja wa klabu ya Man Utd Sir Alex Ferguson amethibitisha taarifa za kuwa na uhakika wa kumsajili kipa wa kimataifa toka nchini Denmark pamoja na klabu ya Aalesund FK ya nchini Norway Anders Lindegaard.
Sir Alex Ferguson ametoa uthibitisho huo kufuatia mazungumzo kati ya Man Utud pamoja na klabu ya Aalesund FK kuonyesha muelekeo wa kupatikana muafaka ambao huenda ukaiwezesha klabu ya Man Utd kukamilisha utaratibu wa usajili ndani ya majuma matatu ama manne yajayo.
Hata hivyo wakati Man utd wakiwa na matumaini ya kumsajili kipa huyo mwenye umri wa miaka 26, kipa wa zamani wa klabu hiyo toka nchini Denmark Peter Schmeichel amepinga hatua ya kumsajiliwa kwa Lindegaard huku akitoa sababu kwa kusema hana uwezo wa kutosha wa kuwatumikia mashetani wekundu.
Man Utd wapo katika mchakato wa kumsaka kipa, kufuatia kipa wao wa sasa Edwin van der Sar kutangaza kustahafu soka baada ya msimu huu kumalizika huku kipa namba mbili Tomasz Kuszczak akishindwa kuaminiwa kurithi nafasi ya kipa huyo toka nchini Uholanzi.
No comments:
Post a Comment