
Kiungo wa kimataifa toka nchini Wales pamoja na klabu ya Arsenal Aaron Ramsey jana amerejea uwanjani kwa mara ya kwanza na kufanikiwa kucheza dakika 45 za mchezo uliowashirikisha wachezaji wa akiba wa Wolves dhidi ya The Gunners.
Aaron Ramsey ambae alikua nje ya uwanja toka mwezi wa pili mwaka huu baada ya kuvunjika mguu ametimiza hatua ya kurejea kwake huku akionyesha kiwango kizuri ambacho kiliisaidia timu yake kupata ushindi wa mabao mawili kwa sifuri.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 19 alivunjika mguu baada ya kuchezewa ovyo na kiungo wa Stoke City Ryan Shawcross wakati Arsenal walipofanya safari ya kwenda Britannia Stadium kusaka point tatu muhimu za ligi kuu msimu uliopita.
Kurejea kwa Aaron Ramsey kunaweza kukifanya kikosi cha Arsenal kupata nguvu zaidi katika nafasi ya kiungo ambayo jana imempoteza Cesc Fabregas baada ya kuumia nyonga.
No comments:
Post a Comment