KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, November 25, 2010

MGOMO WA MAREFA SCOTLAND WAENDELEA.


Chama cha soka nchini Scotland kimethibitisha kuendelea kwa mgomo uliotangazwa na chama cha waamuzi wa soka nchini humo ambao utaathiri ratiba ya michezo ya ligi ya mwishoni mwa juma hili.

Taarifa za chama cha soka nchini humo kutambua uwepo wa mgomo wa waamuzi zimetolewa na mtendaji mkuu Stewart Regan ambapo amesema suala hilo linaendelea kuwasumba vichwa toka mwanzoni mwa juma hili.

Stewart Regan amesema bado wanaendelea na juhudi za kufanya mazungumzo na viongozi wa chama cha waamuzi nchini Scotland kwa lengo la kupata muafaka ambao huenda ukaifanya michezo ya ligi kuendelea mwishoni mwa juma hili.

Waamuzi wa soka nchini Scotland walifikai maamuzi ya kugomea michezo ya ligi kuu nchini humo baada ya kukutana mwishoni mwa juma lililopita kujadili masuala mbali mbali ambayo yamekua yakiwakwanza.

Suala kubwa ambalo lilionekana kuwa kikwazo kwa waamuzi hao hadi kufikia maamuzi ya kugomea michezo ya ligi kuu, ni vitisho na manyanyaso yanayotolewa na mashabiki wa baadhi ya klabu za soka nchini humo ambao mara kadhaa wamekuwa hawaridhishwi na maamuzi yayotolewa uwanjani.

No comments:

Post a Comment