
Kikosi cha klabu ya Sunderland kinahofiwa huenda kikayumba katika michezo ya ligi kuu ya soka nchini Uingereza kufuatia baadhi ya wachezaji wake kukabiliwa na majeraha katika kipindi hiki.
Wachezaji wnaopelekea hofu hiyo ni Titus Bramble pamoja na Michael Turner ambao wote kwa pamoja wanacheza kwenye safu ya ulinzi ambayo imekua ikifanya vyema katika michezo ya msimu huu.
Taarifa iliyotolewa hii leo na uongozi wa klabu hiyo zimeeleza kuwa Bramble ambae hakuwepo kwenye kikosi kilichocheza siku ya jumatatu dhidi ya Everton hii leo alitarajiwa kufanyiwa upasuaji wa goti ambalo limekua likimsumbua kwa muda wa majuma mawili sasa.
Hatua hiyo ya kufanyiwa upasua itamuweka nje ya uwanja Bramble kwa kipindi kirefu ambacho kinatabiriwa kufikia mwezi mmoja na nusu.
Kwa upande wake Michael Turner nae alitarajia hii leo kumuona daktari kwa ajili ya kujua hatma ya maumivu ya goti yanayoendelea kumsumbua na ikiwezekana huenda akafanyiwa upasuaji pia.
Wachezaji wengine ambao ni majeruhi ndani ya kikosi cha Sunderland Darren Bent, Danny Welbeck pamoja na Gyan Asamoah.
No comments:
Post a Comment