KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, November 25, 2010

Steven Gerrard BADO MAJERUHI.


Meneja wa klabu ya Liverpool Roy Hodgson amesema hana haraka ya kumchezesha kiungo na nahodha wake Steven Gerrard ambae kwa sasa anasumbuliwa na maumivu ya nyonga toka kati kati ya juma lililopita.

Roy Hodgson ametoa msimamo huo kufuatia hali ya Steven Gerrard kuanza kuridhisha baada ya kufanyiwa matibabu ambayo yanahisiwa huenda yakamrejesha uwanjani kwa uharaka zaidi mbali na ilivyokua inafikiria kwamba atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa majuma manne.

Meneja huyo pia amelazimika kutoa msimamo huo kwa lengo la kukanusha taarifa zilizotolewa katika vyombo vya habari ambapo zimeeleza huenda akamchezesha kiungo huyo mwishoni mwa juma hili pale kikosi chake kitakapofanya safari ya kuelekea jijini London kucheza na Tottenham Hotspours.

Hata hivyo Roy Hodgson amekiria kuchagizwa na hatua ya kurejea kwa kiungo Joe Cole ambae atamtumnia katika mchezo huo wa mwishoni mwa juma hili.

Katika mchezo huo dhidi ya Spurs Roy Hodgson pia ana matarajio makubwa ya kumtumia winga mahiri toka nchini uholanzi Ryan Babel baada ya kuridhishwa na hatua ya kurejea tena kwa kiwango chake cha kawaida.

No comments:

Post a Comment