KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, November 25, 2010

TUNASTAHILI KUWA HAPA - Harry Redknapp


Baada ya ushindi wa mabao matatu kwa sifuri mbele ya Wender Bremen ya nchini Ujerumani ambao unawavusha kutoka kwenye hatua ya makundi hadi katika hatua ya 16 bora ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya, meneja wa klabu ya Tottenham Harry Redknapp amewapongeza wachezaji wake kwa kazi nzuri waliyoifanya toka walipoanza harakati za kusaka mwanya wa kusonga mbele.

Harry Redknapp meneja pekee alieiwezesha Spurs kucheza michuano ya ligi ya mabingwa amesema kwa hakika wachezaji wake wamekua wakionyesha hali ya kujituma wanapokua uwanjani na jana imedhihirika wazi kwamba walichokua wanakisaka kimepatikana.

Amesema wakati hatua ya makundi ilipokuwa inapangwa mjini Monaco nchini Ufaransa mashabiki wengi ulimwenguni waliwabeza baada ya kuangukia katika kundi la kwanza lenye klabu za Inter Milan, Fc Twenty pamoja na Weder Bremen lakini hawakuvunjika moyo bali walitambua nini wanachotakia kukifanya.

Harry Redknapp pia amezungumzia mchezo wa jana dhidi ya Weder Bremen ambapo amesema kwa ujumla wachezaji wake walionyesha uwezo wa kutosha achilia mbali suala la winga wake wa kimataifa toka nchini Wales Gareth Bale kukosa mkwaju wa penati katika kipindi cha pili.

Nae nahodha wa kikosi cha Spurs Luca Modric amesema juhudi zao na kujituma zaidi ndio chanzo cha kufikia mafanikio ya kucheza hatua ya 16 bora ambayo amedai ni ngumu zaidi hivyo itawalazimu kaza buti.

Modric kiungo wa kimataifa toka nchini Croatia ambae alikua mmoja wa wachezaji walipachika mabao matatu katika mchezo wa jana, pia ametoa shukurani kwa mashabiki wao ambao katika kipindi chote cha kusaka point tatu muhimu za hatua ya makundi walikua pamoja hadi kufikia sasa ambapo wametimiza malengo ya kusonga mbele huku wakisaliwa na mchezo mmoja wa kundi la kwanza dhidi ya Fc Twenty ya nchini Uholanzi.

Katika hatua nyingine meneja wa zamani wa Spurs Gland hoddle amekimwagia sifa kikosi cha klabu hiyo kwa kazi nzuri waliyoifanya na kufanikia kuandika historia mpya huko White Heart Land.

Amesema kwa soka safi lililoonyeshwa na kikosi cha klabu hiyo toka mwanzoni mwa michuano ya ligi ya mabingwa msimu huu kinastahili kupata mafanikio hayo na hapo walipofika ndipo mahala pake huku akigusia mchezo dhidi ya Inter Milan uliochezwa mjini Milan na kukamalizika kwa Spurs kuchapwa maboa manne kwa matatu.

Ushindi wa mabao matatu kwa sifuri uliopatikana jana kwenye uwanja wa White Hert Lane unaifanya Spurs kufikisha point 10 sawa na vinara wa kundi hilo Inter Milan.

No comments:

Post a Comment