
Meneja wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger ameonyesha kuchukizwa na maamuzi yaliyotolewa kwenye mchezo wa usiku wa kuamkia hii leo ambao ulishuhudia kikosi chake kikibamizwa mabao mawili kwa sifuri huko mjini Braga nchini Ureno.
Wenger amesema hakuona sababu za msingi zilizomfanya muamuzi wa mchezo huo kumuonyesha kadi ya njano mshambuliaji wake Carlos Vella ambae alichezewa rafu katika eneo la hatari.
Amesema mbali na kushangazwa na maamuzi hayo pia anashindwa kuelewa nini kazi ya muamuzi wa nyuma ya goli ambae alitakiwa kumshawishi muamuzi wa kati kuamurui mkwaju wa paneti kutokana na yeye kuwa karibu na kitendo hicho lakini alishindwa kutimiza wajibu wake.
Akizungumzia kuumia kwa kiungo na nahodha wa kikosi chake Cesc Fabregas, Arsene Wenger amesema kiungo huyo wa kimataifa toka nchini Hispania amepata maumivu ya nyonga na hafahamu ni muda gani atakuwa nje ya uwanja huku taarifa zilizotolewa muda mchache uliopita zikieleza kwamba huenda ikamchukua muda wa majuma matatu yajayo kurejea tena uwanjani.
Pia mzee huyo wa kifaransa ameuzungumzia mchezo wa jana kwa ujumla huku akibainisha kuwa wapinzani wao walicheza kwa kujihami zaidi na walitumia nafasi mbili walizozipata na kutimiza malengo yao ya ushindi.
No comments:
Post a Comment