

Shirikisho la soka barani ulaya UEFA huenda likachunguza kitendo kilichopelekea wachezaji wawili wa Real Madrid kuonyeshwa kadi nyekundu katika mchezo wa jana ambao uliwakutanisha na mabingwa wa zamani wa Ulaya Ajax Amsterdam.
UEFA wanatazamiwa kufanya uchunguzi wa kitendo hicho kilichopelekea kuonyeshwa kadi nyekundu kwa Xavi Alonso pamoja na Sergio Ramos huku dakika nne zikiwa zimesalia mchezo huo kumalizika.
Kitendo hicho kimezua maswali kadhaa kwa mashabiki wa soka ulimwenguni waliokua wakiufuatilia mchezo huo ambapo wengi wao wamedai wachezaji hao wamefanya makusudi huku wakitambua tayari klabu yao imeshafanikiwa kutinga kwenye hatua ya 16 bora ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.
Ruud Gullit pamoja na Gland Hoddle ni wachezaji waliofanikiwa kutamba na baadhi ya vilabu vya soka barani Ulaya wamelijadili jambo hilo ambapo wameonyesha kuziunga mkono kauli zinazotolewa na mashabiki wengine wa mchezo wa soka ulimwenguni kote.
No comments:
Post a Comment