KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, December 8, 2010

Alan Pardew AINGIA KWENYE KINYANG'ANYIRO.


Heka heka za kumsaka mrithi wa Chris Hughton huko St Jame’s Park zinaendelea huku uchunguzi ukionyesha kwamba meneja wa zamani wa klabu Reading, West Ham, Charlton Athletic pamoja na Southampton Alan Pardew akitajwa huenda akatangazwa kuwa meneja mpya wa klabu ya Newcastle ndani ya saa 24 zijazo.

Uchunguzi uliofanywa na shirika la utangazaji la nchini Uingereza BBC umeonyesha kwamba Alan Pardew ana nafasi kubwa kufuatia uongozi wa The Magpies kutangaza kuhitaji meneja mwenye uzoefu na ligi kuu ya soka nchini Uingereza.

Mpaka sasa meneja huyo mwenye umri wa miaka 49 ana sifa ya zaidi ya michezo 500 ya ligi kuu ambayo ameitumia akiwa na klabu alizozifundisha.

Mbali na uchunguzi huo, pia yasemekana Alan Pardew siku kumi zilizopita alikuwa na mazungumzo ya faragha na mmiliki wa klabu ya Newcastle Utd Mike Ashley pamoja na mkurugenzi wa klabu hiyo Derek Llambias, mazungumzo yaliyofanyika katika jumba la kuchezea kamari la London Casino.

Nafasi hiyo ya umeneja ndani ya klabu ya Newcastle Utd pia inawaniwa na meneja wa zamani wa klabu ya Aston Villa Martin O'Neill pamoja na Martin Jol, alietangaza kuachana na klabu ya Ajax Amsterdam siku mbili zilizopita.

No comments:

Post a Comment