KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, December 8, 2010

Cesc Fabregas pamoja na Abou Diaby WAONYESHA MATUMAINI.


Nahodha na kiungo wa klabu ya Arsenal Cesc Fabregas pamoja na Abou Diaby wamerejea mazoezini baada ya kupona majeraha yaliyokua yakiwakabili kwa majuma kadhaa yaliyopita.

Viungo hao wawili wamerejea katika mazoezi na wachezaji wenzao huku wakilenga kujumuishwa katika klikosi cha klabu ya Arsenal ambacho mwanzoni mwa juma lijalo kitaifunga safari kulekea Old Trafford kucheza na wenyeji Man Utd katika mchezo wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza.

Fabregas alikuwa nje ya uwanja kwa majuma mawili yaliyopita, kufuatia majeraha ya nyama za paja aliyoyapata akiwa kwenye mchezo wa tano wa hatua ya makundi wa ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya FC Braga.

Diaby nae amekua nje kwa kipindi cha majuma 12 yaliayopita, kufuatia maumivu ya kifundo cha mguu aliyoyapata katika mchezo wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza uliochezwa Septemba 11 ambapo Arsenal walionyeshana undava na Bolton Wanderers na kufanikiwa kupata ushindi wa mabao manne kwa moja.

No comments:

Post a Comment