
Shirikisho la soka duniani kote FIFA limetoa kauli ya kujibu tuhuma zilizotolewa na baadhi ya wadau wa mchezo huo toka nchini Uingereza siku baada ya nchi hiyo kukosa nafasi ya kuwa mwenyeji wa fainali za kombe la dunia za mwaka 2018.
FIFA wametoa kauli hiyo kupitia kwa katibu mkuu Jérôme Valcke walipokutana na waandishi wa habari huko falme za kiarabu alipokua akizungumzia michuano ya klabu bingwa duniani iliyoanza kutimua vumbi lake huko Abu dhabi muda mchache uliopita.
Jérôme Valcke amesema FIFA wamesikia vilio vya waingereza ambao wamelitaka shirikisho hilo kubadili mfumo wa wajumbe wa kamati ya utendaji ambao ndio wenye dhamana ya kuzipigia kura nchi zilizoomba kuandaa fainali za kombe la dunia lakini wasitarajie vilio vyao vitasikilizwa kwa hivi sasa kama wanavyotaka wao.
Amesema FIFA haiwezi kubadili mfumo kwa maneno yanayozungumzwa baada ya kupatikana washindi wa kuandaa fainali za kombe la dunia za mwaka 2018 pamoja na 2022 bali itafanya hivyo kwa maamuzi binafsi.
Jérôme Valcke pia amewataka waingereza kujifunza namna ya kushindwa na kushinda katika kinyang’anyiro chochote watakachowania na ifahamike hawakua pekee yao walioshindwa bali zilikua nchi nyingi zilizoomba na zimeshindwa.
Wakati huo huo kiungo wa kimataifa toka nchini Urusi na klabu ya Arsenal ya nchini Uingereza Andrey Ashavin ameendelea kuonyesha furaha yake baada ya nchi ya Urusi kutangazwa mshindi wa kinyang’anyiro cha kuwa mwenyeji wa fainali za kombe la dunia za mwaka 2018.
Amesema aliporejea jijini London akitokea mjini Zurich nchini Uswiz alipokwenda kuungana na mabalozi waliokua wakiipigia debe urusi ili iweze kushinda, wachezaji wenzake kama Jack Wilshere walimpongeza huku wakimtania ni nini alichokifanya mpaka ikafikia hatua wakashinda nafasi hiyo.
Amesema kiungo huyo kinda wa nchini Uingereza hupenda kumtania kwa kumueleza wazi kwamba yeye binafsi alikua amejiandaa kutwaa ubingwa wa dunia mwaka 2018 mbele ya mashabiki wa nyumbani kwao.
No comments:
Post a Comment