
Uongozi wa klabu ya Newcastle Utd umethibitisha Alan Pardew kuwa meneja wa kikosi cha klabu hiyo iliyorejea kwenye harakati za kusaka ubingwa wa nchini Uingereza baada ya kufanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi daraja la kwanza msimu uliopita.
Pardew ametangazwa kuwa meneja wa klabu hiyo, huku saa 24 zikiwa zimepita baada ya uchunguzi wa shirika la utangazaji la nchini Uingereza BBC kubaini meneja huyo alikua na nafasi kubwa ya kuchukua madaraka huko St Jame’s Park.
Uongozi wa The Magpies umefikia hatua ya kumtangaza Alan Pardew hii leo baada ya kumalizana nae ambapo picha za siri za televisheni zilionyesha viongozi wa klabu ya Newcastle Utd pamoja na meneja huyo wa kiingereza wakiwa kwenye kikao cha faragha kwenye moja ya hoteli huko jijini London.
Taarifa iliyotolewa mapema hii leo kwa saa za nchini Uingereza zimethibitisha kwamba Alan Pardew ameingia mkataba wa kukinoa kikosi cha klabu ya Newcastle Utd kwa muda wa miaka sita ijayo huku akitakiwa kutimiza malengo yaliyowekwa klabuni hapo.
Hata hivyo baadhi ya mashabiki wa Newcastle Utd wameonyesha kutokukubalia na uteuzi wa meneja huyo ambapo wamesema hana sifa za kutosha kama ilivyo kwa mameneja wengine waliokua wakitajwa huenda wangechukua nafasi ya Chris Hughton alietimuliwa kazi mwanzoni mwa juma hili.
Kukutaliwa kwa meneja huyo na baadhi ya mashabiki wa klabu ya Newcastle Utd kumezunguziwa tofauti na muandishi wa habari wa gazeti la The Sun Shaun Custis ambapo amesema huenda mashabiki hao wakawa na haki ya kuzungumza lolote juu ya kuajiriwa kwa Alan Pardew, lakini akasisitiza kwamba ukweli utaonekana wazi kwa mashabiki wengine wa klabu hiyo pindi meneja huyo atakapoanza kazi yake siku ya kwanza.
Mameneja wengine waliokua wakipigiwa chepuo klabuni hapo kushika pahala pa ni Chris Hughton ni aliekua meneja wa klabu ya Aston Villa Martin O’Neil pamoja na Martin Jole alietangaza kujiuzulu kukinoa kikosi cha Ajax Amsterdam mwanzoni mwa juma hili.
Alan Pardew ataanza kibarua cha kukiongoza kikosi cha klabu ya Newcastle Utd mwishoni mwa juma hili ambapo The Magpies watakuwa nyumbani huko St Jame’s Park wakiwakaribisha majogoo wa jiji Liverpool.
No comments:
Post a Comment