KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, December 9, 2010

Johan Elmander AWAUMIZA VICHWA BOLTON.


Mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Sweden na klabu ya Bolton Wanderers Johan Elmander anahofiwa huenda akagoma kusaini mkataba mpya na klabu hiyo kufuatia mkataba wake wa sasa kutarajia kufikia kikomo mwishoni mwa msimu huu.

Hofu kwa mshambuliaji huyo zimekuja kufuatia baadhi ya vilabu vingi barani Ulaya kuonyesha hatua nzito za kutaka kumsajili kwa hali na mali kufuatia kuonyesha umahiri mkubwa na kusaidia klabu hiyo kupata ushindi katika baadhi ya michezo ya ligi.

Tayari uongozi wa klabu ya Bolton Wanderers umeshafungua milango ya mazungumzo kwa mshambuliaji huyo kabla ya dirisha dogo la usajili halijafunguliwa mwezi januari mwaka 2011, lakini Johan Elmander amesema bado anafikiria kuingia katika utaratibu wa mazungumzo hayo ya kusaini mkataba mpya na siku za hivi karibuni anatarajia kutoa msimamo wake binafsi.

Johan Elmander pia akaongeza kwamba yeye si mchezaji ambae anafikiria sana pesa bali ni mchezaji anapenda maendeleo yake binafsi kwa ajili ya kujisaidia mwenyewe na kuwasaidia wale walio nyuma yake pia.

Johan Elmander alisajiliwa na klabu ya Bolton Wanderes mwaka 2008 kwa ada ya uhamisho wa paund million 8 akitokea nchini Ufaransa alipokua akiitumikia klabu ya Toulouse.

No comments:

Post a Comment