
Meneja wa klabu bingwa nchini Uingereza Chelsea Carlo Ancelotti amesema bado ana sifa za kutosha za kuendelea kuwa meneja wa klabu hiyo licha ya matokeo mabovu kuendelea kumuandama.
Carlo Ancelotti ametoa kauli hiyo usiku wa kuamkia hii leo mara baada ya mchezo wa ligi ya mabingwa barani ulaya uliochezwa huko nchini Ufaransa ambapo mabingwa wa soka nchini humo Olympic Marseille walifanikiwa kuchomoza na point tatu muhimu baada ya kupata ushindi wa bao moja kwa sifuri.
Akitao sababu za kuhisi bado ana umuhimu wa kuendelea kuwa meneja huko Stamford Bridge, mzee huyo wa kitaliano amesema kikosi chake bado kipo imara na kimekua kikicheza soka la kiushindani lakini kimekua hakina bahati ya ushindi.
Amesema licha ya matokeo kuendelea kuwa mabovu kwa upande wao, bado anaamini kikosi chake kinapata uzoefu wa kutosha ambao ana matumaini utakisaidia katika mchezo wa mwishoni mwa juma hili ambapo wanakwenda kukutana na Tottenham Hotspurs huko White Hart Lane jijini London.
Nae baki na nahodha wa klabu ya Chelsea John Terry ameyaunga mkono maneno yaliyozungumzwa na meneja wake Carlo Ancelloti huku akiendelea kusisistiza suala la kuendelea kupata uzoefu ambao unawarejesha katika hali yao ya kawaida ambapo wana matumaini ya kufanya vizuri katika mchezo wa mwishoni mwa juma hili.
Chelsea wamepoteza point tatu za mchezo wa jana ambazo zimewapa nafasi ya kufuzu mabingwa wa soka nchini ufaransa Olympic Marseille ambao wanajiunga na vilabu vingine 15 vilivyotinga katika hatua ya mtoani ya ligi ya ambingwa barani Ulaya.
No comments:
Post a Comment