KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, December 10, 2010

BADO WATAENDELEA KUWA KATIKA HIMAYA YA LIVERPOOL.


Roy Hodgson amezungumzia mikakati ya kiungo wa kimataifa toka nchini Brazil Lucas Pezzini Leiva ambae yu kwenye harakati za kusiani mkataba mpya utakaoendelea kumuweka huko Anfiled.

Amesema kwa sasa mazungumzo kati ya uongozi wa klabu ya Liverpool na wakala wa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 23 yanaendelea kufanyika na matumaini ya kufanikiwa yanaonekana.

Lucas Pezzini Leiva amekuwa katika mipango ya kutaka kusajiliwa na klabu ya Sevilla ya nchini Hispania kwa lengo la kutaka kuziba nafasi ya kiungo wa kimataifa toka nchini Italia Tiberio Guarente alie majeruhi.

Roy Hodgson pia amewaelezea mashabiki na wapenzi wa klabu ya Liverpool juu ya mipango iliyowekwa klabuni hapo kwa ajili ya beki wa kulia wa klabu hiyo Glen Johnson ambae siku za hivi karibuni aliliripotiwa huenda akaondoka na kuelekea nchini Italia kujiunga na meneja wake wa zamani Rafael Benitez.

Amesema beki huyo wa kiingereza bado yupo kwenye mipango yake na sasa wanaendelea na mazungumzo ya kusaini makataba mpya kufuatia mkataba wake wa sasa kutarajia kufikia kikomo mwishoni mwa msimu huu.

No comments:

Post a Comment