
Meneja wa klabu ya Wigan Atheletic Roberto Martinez nae ameeleza mikakati yake huku akisema majeruhi alionao kwa sasa bado hawajamshawishi kufikiria kufanya usajili wa wachezaji wengine kwa lengo la kuziba nafasi zao.
Amesema wachezaji walio nao kwa sasa bado anaawaamini wanaweza kuziba nafasi za wengine ambao wanauguza majeraha na haoni sababu ya kushawishika kufanya hivyo, kwa kuhofia ushindani uliopo katika mashindano anayoshiriki.
Kwa sasa Roberto Martinez anakabiliwa na wachezaji majeruhi kama Franco Di Santo na James McCarthy (kifundo cha mguu) Victor Moses (bega) pamoja na nahodha Gary Caldwell (Paja).
No comments:
Post a Comment