
Kiungo wa kimataifa toka nchini Uingereza na klabu ya LA Galax ya nchini Marekani David Beckham ameungana na waziri mkuu wa nchini Uingereza David Cameron kumtaka raisi wa FIFA Sepp Blatter kutozipa nafasi tuhuma hizo za kupokea mlungula.
David Beckham pamoja na David Cameron ambao wote kwa pamoja wapo kwenye kamati ya kuipigia debe nchi Uingereza ili iweze kuwa mwenyeji wa fainali za kombe la dunia za mwaka 2018 wamemtaka kiongozi huyo pamoja na kamati kuu ya FIFA kufikiria kilicho mbele yao ambacho ni upigaji wa kura utakaofanyika kesho mjini Zurich nchini Uswiz.
Beckham amesema kwa sasa hakuna muda wa kupoteza kuanza kufikiria masuala ya kipuuzi kama yaliyodaiwa na kipindi cha PANORAMA na badala yake ni kuhakikisha FIFA wanapewa nafasi yao ya kuamua ni nchi gani itaandaa fainali za kombe la dunia za mwaka 2018 pamoja na 2022.
Beckham pia amezungumzia kuwa na imani mna wajumbe watakaopiga kura hiyo kesho huku akiamini wataiwezesha nchi ua Uingereza kuwa mwenyeji wa fainali za kom,be la dunia za mwaka 2018.
Nae waziri mkuu wa nchini Uingereza David Cameron ameonekana kuwa na matumaini makubwa na nchi yake kupata nafasi ya kuwa mwenyeji wa fainali za kombe la dunia za mwaka 2018, huku akitamba mambo waliyoyawasilisha FIFA yana mvuto zaidi ya wapinzani wao.
Nchi zinazowania kuandaa fainali za kombe la dunia za mwaka 2018 ni Uingereza,Urusi, Hispania kwa kushirikiana na Ureno pamoja na nchi ya Uholanzi kwa kushirikliana na Ubelgiji.
Na nchi zinazowania kuandaa fainali za kombe la dunia za mwaka 2022 ni Australia, Japan, Qatar, Korea Kusini pamoja na Marekani.
No comments:
Post a Comment