KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, December 1, 2010

Issa Hayatou KUIFIKISHA MAHAKAMANI BBC.


Raisi wa shiriksiho la soka barani Afrika CAF ambae pia ni mjumbe wa kamati kuu ya shirikisho la soka duniani FIFA Issa Hayatou amekanusha vikali kuhusika na masuala ya kupokea mlungula kama ilivyodaiwa jana kupitia vyombo mbali mbali vya habari.

Issa Hayatou amekanusha vikali kuhusika na masuala la kupokea mlungula, baada ya kujumuishwa kwenye matokeo ya uchunguzi uliofanywa na kipindi cha Panorama ambacho hurushwa na shirika na utangazaji la nchini Uingereza BBC.

Katika kipindi cha PANORAMA kilichorushwa hewani siku ya jumatatu ya juma hili, ilidaiwa kuwa Issa Hayatou ambae pia ni makamu wa raisi wa FIFA, mnamo mwaka wa 1995 alipewa mlungula wa franga za kifaransa 100,000 ambazo ni sawa na paund za kiingereza 12,900, kutoka kwenye kampuni moja ya nchini Uswizi kwa lengo la kampuni hiyo ipewe mkataba mnono wa matangazo na FIFA.

Katika utetezi wake Hayatou amesema pesa hizo kweli zilitolewa na kampuni hiyo lakini kwa matumizi rasmi ya maadhimisho ya miaka arobaini ya shirikisho la soka barani Afrika CAF na si kama ilivyodaiwa kwenye kipindi cha Panorama cha BBC.
Hata hivyo Issa Hayatou amedai atalifikisha mahakamani shirika la utangazaji la nchini Uingereza BBC kwa tuhuma alizotupiwa.

Katika rapsha hiyo ya mlungula Issa Hayatou alijumuishwa na wajumbe wengine wawili ambao ni Nicolas Leoz wa nchini Paraguay pamoja na Ricardo Teixeira kutoka nchini Brazil.

Viongozi hao watatu wapo kwenye jopo litakalopiga kura kesho ya kuamua nchi zitakazoandaa fainali za kombe la dunia za mwaka 2018 na 2022.

No comments:

Post a Comment