
Meneja wa klabu ya Newcastle Utd Chris Hughton jana alilazimika kuwafungia wachezaji wake kwenye chumba cha kubadilishia baada ya kuchukizwa na matokeo mabovu yaliyopatikana kwenye mchezo wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza dhidi ya West Bromwich Albion.
Meneja huyo amesema kabla ya kufanya kitendo hicho aliwataka wachezaji wake kueleza sababu zilizopelekea kubamizwa mabao matatu kwa moja katika mchezo huo lakini hakupatiwa majibu ya haraka hivyo ilimlazimu kufanya hivyo kwa lengo ya kukipa nafasi kikosi chake kujadili kwa muda.
Kitendo cha wachezaji wa Newcastle kufungiwa kwenye chumba cha kubadilishia kilichukua muda wa saa moja na kisha Chris Hughton alilazimika kuwafungulia pasipo kuhitaji jibu lolote.
Alipohojiwa na vyombo vya habari kwa nini amefanya hivyo, Chris Hughton alisema alilazimika kufanya hivyo kwa lengo la kuwataka wachezaji wake wafahamu umuhimu wao katika klabu ya Newcastle ambayo inahitaji mafanikio kama ilivyokua kwenye msimu wa ligi uliopita ambapo walimaliza vinara katika ligi daraja la kwanza.
Amesema msimu huu umekua mbovu kwao kufuatika matokeo kutokua mazuri ambapo kila juma wanapocheza kikosi chake kimekua na kasumba ya kama homa za kupanda na kushuka hatua mbayo ameitaja kuwa sio nzuri kwao.
Mpaka sasa Newcastle Utd wameshashuka dimbani mara 16, wameshinda michezo mitano, wamepoteza michezo 7, wametoka sare michezo minne na wanashikilia nafasi ya 11 kwenye msimamo wa ligi.
No comments:
Post a Comment