
Uongozi wa klabu ya Newcastle United umetangaza kumtimua kazi meneja wa klabu hiyo Chris Hughton sambamba na kocha wa makipa wa klabu hiyo Paul Barron.
Uongozi wa klabu ya Newcastle Utd umefikia maamuzi ya kumtimua kazi Hughton, baada ya mkutano wa bodi uliofanyika jana na kufikia maamuzi hayo ambayo hata hivyo hayajaelezwa nini sababu ya kutimuliwa kwa meneja meneja huyo.
Taarifa rasmi iliyotolewa na uongozi wa klabu hiyo mara baada ya kikao cha bodi zilionyesha kumshukuru Cris Hughton kwa mchango mkubwa alioutoa klabuni hapo na kumtakia kila la kheri huko aendapo.
Katika utawala wake toka msimu uliopita akiwa kama meneja mkuu wa klabu ya Newcastle, Chris Hughton alionyesha kujituma kwa hali ya juu na kufanikiwa kuchukua ubingwa wa ligi daraja la kwanza ambao aliwarejsha katika ligi kuu ya soka nchini humo msimu huu.
Akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kupewa ruhusa ya kuondoka klabuni hapo Chris Hughton ambae amekua kwenye madaraka kamili ya umeneja kwa kipindi cha miezi 18 iliyopita amesema hana budi kukujishukuru yeye binafsi kwa kazi nzuri aliyoifanya ndani ya klabu hiyo na ana imani kubwa mchango wake utaendelea kukumbukwa na kuheshimiwa pia.
Kutimuliwa kazi kwa meneja huyo kumekuja siku moja baada ya kikosi cha Newscastle Utd kutembezewa kichapo cha mabao matatu kwa moja dhidi ya West Brom Albion.
No comments:
Post a Comment