
Kikosi cha Arsenal kitaendelea kumkoa beki Thomas Vermaelen ambae kwa kipindi cha miezi mitatu amekua nje ya uwanja kufuatia maumivu ya kisigino yanayomkabili kwa kiasi kikubwa.
Taarifa zilizotolewa hii leo na meneja wa klabu hiyo Arsene Wenger zimeeleza kwamba beki huyo mwenye umri wa miaka 24 hatorejea uwanjani kwa hivi sasa na badala yake huenda akaonekana tena uwanjani mwanzoni mwa mwaka 2011.
Wenger amesema beki huyo bado anaendelea kusumbuliwa na maumivu ya kisigino hivyo ameendelea kushauriwa kuwa nje ya uwanja kwa lengo la kupatiwa matibabu zaidi ambayo yatamuwezesha kurejea kwenye hali yake ya kawaida.
Amesema walikua wakimuhitaji kwa udi na uvumba katika kipindi hiki cha ushindani mkali lakini kwa ushaiuri waliopatiwa na jopo la madatari wameona kuna umuhimu wa kuendelea na matibabu na wana imani atarejea uwanjani akiwa vizuri na kuisaidia Arsenal ambayo ina malengo makubwa msimu huu.
Hatua ya kuwa nje kwa beki huyo wa kimataifa toka nchini Ubelgiji, imempa nafasi ya kutosha beki wa kifaransa Sebastian Squillaci ambae mpaka sasa ameshaanzishwa katika kikosi cha kwanza mara 18 kwa kushirikiana na beki mwingine wa kifaransa Laurent Koscielny.
Mbali na Thomas Vermaelen kuwa nje kwa majeraha pia mzee Arsene Wenger akaendelea kuthibitisha taarifa za kumkosa nahodha na kiungo wake Cesc Fabregas pamoja na Abou Diaby ambao wote kwa pamoja ni majeruhi.
Wakati huo huo beki wa pembeni wa zamani wa klabu ya Arsenal Nigel Winterburn ameelezea imani yake kwa kikosi cha klabu ya Arsenal ambacho kimepata nafasi ya kuongoza kwenye msimamo wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza baada ya kuibamiza klabu ya Fulham huku Chelsea aking’ang’aniwa na Everton mwishoni mwa juma lililopita.
Nigel Winterburn amesema anaamini endapo wachezaji wa klabu ya Arsenal wataendelea na mfumo wa kushinda katika michezo yao sambamba na kusikiliza maagizo ya meneja wao Arsene wenger kuna kila sababu msimu huu klabu hiyo ikafanikiwa kuurejesha ubingwa wa nchini Uingereza ambao umewapotea kwa miaka mitano iliyopita.
No comments:
Post a Comment