KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, December 3, 2010

David Gold AZUNGUMZIA MASKIKITIKO YAKE.


Waziri mkuu wa nchini Uingereza David Cameron ameelezea masikitiko yake baada ya nchi hiyo kukosa nafasi ya kuandaa fainali za kombe la dunia za mwaka 2018 kufuatia kura zilizopigwa na wajumbe wa kamati kuu ya shirikisho la soka duniani kote FIFA hapo jana.

David Cameron ambae alikua mmoja wa mabalozi wa kuipigia debe nchi ya Uingereza ili iweze kupata nafasi hiyo amesema hatua ya kukosa uenyeji wa fainali za kombe la dunia za mwaka 2018 kwa hakika imemuhuzunisha sana lakini hakusita kuisifia nchi ya Urusi iliyoibuka kidedea kwenye kinyang’anyiro hicho.

Hata hivyo David Cameron bado anaamini ombi lao waliloliwakilisha FIFA lilikua na kila sababu ya kushinda lakini bado maamuzi yalisalia kwa wajumbe ambao ndio wenye makali ya kuamua nchi ipi iandae fainali hizo.

Mbali nay eye binafsi kuamini ombi lao liolikua na uzito mkubwa, pia akabainisha mawili matatu waliyoelezwa na FIFA ambapo amesema nao walipendezewa na mambo yao ambayo yalikua na uzito mkubwa katika kila idara.

David Cameroon pia amewashukuru wajumbe wenzake walioongozana huko mjini zurich nchini Uswiz ambao ni David Beckham pamoja na Prince Willium kwa ushirikiano mzuri waliouonyesha sambamba na hotuba waliyoitoa kwa wajumbe kabl ya zoezi la kura halijaanza kuchukau mkondo wake.

Katika hatua nyingine kiongozi huyo wa nchini Uingereza amewataka wananchi wan chi hiyo kuwa watulivu na katika kipindi hiki cha masikitiko huku akiwasisitiza kutoanza kumfikiria mchawi.

Nae kiungo wa kimataifa kutoka nchini Uingereza David Beckham amezipongeza nchi za Urusi pamoja na Qatar kwa ushindi mzuri walioupata ambao sasa unawawezesha kutembea vifua mbele ulimwengu mzima baada ya kupata nafasi ya kuwa wenyeji wa fainali za kombe la dunia.

Backham nae hakusita kuelezea namna alivyojisikia baada ya Urusi kutangazwa kuwa washindi wa kinyang’anyiro cha kuwa wenyejiw a fainali za kombe la dunia za mwaka 2018.

No comments:

Post a Comment