KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, December 3, 2010

Vladmir Putin ASHANGWEKA !!!!


Wakati Uingereza wakizungumzia masikitoko, waziri mkuu wa nchini Urusi Vladmir Putin ameahidi nchi hiyo itafanya maklubwa katika maandalizi ya fainali za kombe la dunia ambazo zitafanyika kwa mara ya kwanza nchini humo.

Putin ambae alilazimika kuelekea mjini Zurich nchini Uswaz muda mchache kabl ya kutangazwa kwa matokeo ya kura amtoa ahadi hizo mbele ya wajumbe wa kamati kuu ya FIFA.

Amesema watajitahidi kutengeneza viwanja vya kisasa kwa wakati na anaamini kila mmoja atakaekuwepo wakatin huo atafurahia maandalizi watakayoyafanya sambamba na kufurahia utamaduni wa kirusi.

Vladmir Putin pia amewashukuru wajumbe wa kamati kuu ya FIFa kwa kuiwezesha nchi ya Urusi kuwa mwenyeji wa fainali za kombe la dunia za mwaka 2018, huku pia akiwashukuru wapinzani wao walikua wakiiwania nafasi hiyoa mbao ni Uingereza, Hispania kwa kushirikiana na Ureno pamoja na nchi ya Uholanzi kwa kushirikliana na Ubelgiji.

Wakati huo huo mtendaji mkuu wa mabalozi waliokua wakiipigia debe nchi ya Qatar Emir Sheikh Mohammad bin Hamad Al-Thani nae amezungumzia furaha yake ambayo imetokana na nchi yao kuwa ya kwanza kuandaa fainali za kombe la dunia katika ukanda wa mashariki ya kati.

Amesema ushindi wao unawapa changamoto mpya za kuendelea kujipanga vyema na utakapofika wakati kila mmoja ataekwenda kushuhudia fainali hizo nchini Qatar atafurahi.

No comments:

Post a Comment