
Mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Uingereza na klabu ya Wigan Athletic Victor Moses huenda akawa nje ya uwanja kwa takriban majuma matatu yajayo baada ya kuumia bega katika mchezo hatua ya robo fainali ya kombe la ligi dhidi ya Arsenal.
Taarifa toka ndani ya klabu ya Wigan Athletic zimeeleza kuwa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 19 anafikiriwa kuwa nje ya uwanja kwa kipindi hicho baada ya kufanyiwa vipimo ambavyo vimeonyesha namna alivyopata jeraha katika bega lake la mkono wa kushoto.
Taarifa hizo zimeendelea kuanisha kuwa bado kuna uwezekano mkubwa kwa Victor Moses kurejea uwanjani kwa uharaka zaidi kama matibabu yake yatakwenda vizuri.
Meneja wa klabu ya Wigan Athletic Roberto Martinez amesema kukosekana kwa mshambuliaji huyo kwake ni pigo kubwa kutokana na mchango wake anaoutoa uwanjani kila anapompa nafasi lakini akaahidi kuwatumia wachezaji wengine wanaocheza nafasi ya ushambuliaji.
Katika mchezo huo wa hatua ya robo fainali Wigan Athletic walikubali kisago cha mabao mawili kwa sifuri ambacho kimeipa nafasi Arsenal kutinga kwenye hatua ya nusu fainali ya michuano ya kombe la ligi.
No comments:
Post a Comment