KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, December 8, 2010

GFA WAKUTANA KUJADILI MZOZO.


Uongozi wa chama cha soka nchini Ghana umeelezea kusikitishwa na hatua ya maafisa wa kitengo cha kupambana na kuzuia rushwa cha nchini humo cha kuizingira ofisi ya chama hicho hapo jana na kufanya upekuzi usio rasmi.

Akizungumza kwa niaba ya uongozi, msemaji wa GFA Randy Abbey amesema uvamizi huo wa uliofanywa na maafisa wa kitengo hicho cha serikali wao wameuchukulia kama uhalifu ambao hawaukubali nao hata kidogo.

Amesema maafisa hao kubwa walilokua wakilitafua ni nyaraka za mikataba ya kibiashara ambayo GFA wameingia na makampuni mbali mbali kwa ajili ya kuendesha mchezo wa soka nchini humo huku ikidaiwa nyaraka hizo zimekua zikisainiwa kwa taratibu za udanganyifu.

Hata hivyo Randy Abbey amesthibitisha kuwepo kwa mkutano wa dharura wa kamati ya utendaji ya GFA ambao utafanyika hii leo huku ajenda kuu ikiwa ya uvamizi uliofanywa jana na kitengo cha kuzuia na kupambana na rushwa kilicho chini ya serikali ya nchini Ghana.

Zogo hilo la upekuzi wa nyaraka za kibiashara za GFA lililotokea jana katika ofisi za chama cha soka nchini Ghana zilizopo mjini Accra, huenda likaishurutisha FIFA kutoa maamuzi ya kuifungia nchi hiyo ya magharibi mwa bara la Afrika kujihusisha na masuala ya soka la kimataifa kufuatia onyo lililotolewa juma lililopita ambapo nchi nchi hiyo ilitakiwa kutochanganya masuala ya soka pamoja na serikali.

No comments:

Post a Comment