KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, December 7, 2010

GHANA SHUGHULI BADO PEVUUUUUU !!!!


Siku kadhaa kupita baada ya shirikisho la soka duniani FIFA kuionya nchi ya Ghana kutochanganya masuala ya serikali na mchezo wa soka, hali imeendelea kuwa tete nchini humo baada ya hii leo ofisi za chama cha soka nchini humo GFA kuzingirwa na maofisa wa kitengo cha kuzuia na kupambana rushwa.

Sababu kubwa iliyopelekea maafisa hao kuzizingira ofisi za chama hicho imetajwa kuwa ni tuhuma za matumizi mabovu ya fedha yanayofanywa na watendaji wa GFA, hivyo baada ya maafisa hao kufika ndani ya ofisi hizo zilizopo mjini Accra walianza kutafuta nyaraka ambazo hazijaelezwa mpaka sasa zilikua ni za kitu gani.

Licha ya kufanya shughuli za upekuzi, maafasa hao wamechukua komputa pamoja na simu za viganjani za watendaji wa GFA waliokua nje na ndani ya jingo la ofisi, lakini bado haijafahamika ni sababi zipui zilizopelekea vitu hivyo kuchukuliwa.

Mkuu wa kitengo hicho alieongozana na maafisa wenzake alizungumza na vyombo vya habari na kueleza kwamba wamefikia hatua ya kufanya upekuzi kwenye ofisi za GFA kufuatia ruhusa waliyopewa na Mahakam akuu nchini humo.

Hata hivyo wakati wa tukio hilo likitokea Rais wa chama cha soka nchini Ghana GFA, Kwesi Nyantakyi, hakuwepo ofisini hivyo ilikua ni vigumu kwa upande wa viongozi wa soka nchini humo kutoa kauli ya nini kilichopelekea ukaguzi huo kufanyika.

Suala hilo la mahakama kukiamuru kitengo cha kupambana na kuzuia rushwa ambacho kipo chini ya serikali ya nchini humo huenda kikalifanya shirikisho la soka duniani FIFA kufikia maamuzi ya kuifungia Ghana kujihusisha na masuala la soka la kimataifa.

FIFA wanahofiwa kuchukua maamuzi hayo, kufuatia onyo lililotolewa siku za hivi karibuni baada ya uchunguzi uliofanywa kubaini kwamba serikali ya nchini Ghana ilikua inashinikiza jina la Abaid pele lipelekwe kwenye shirikisho la soka barani Afrika ili aweze kuwania nafasi ya ujumbe wa kamati luu, lakini ombi hilo lilikataliwa na GFA.

No comments:

Post a Comment