
Shirikisho la soka barani ulaya UEFA limempunguzi adhabu meneja wa klabu ya Real Madrid José Mário dos Santos Félix Mourinho baada ya kumtoza faini sambamba na kumfungia michezo miwiwli ya michuano ya ligi ya mabingwa barani ulaya baada ya kumkuta na hatia ya kujihusisha na vishawishi vya kuwataka wachezaji wake kuonyeshwa kadi nyekundu kwa makusudi.
UEFA wamempunguzia adhabu meneja huyo wa kireno ambapo sasa itamlazimu kuukosa mchezo mmoja wa ligi ya mbingwa barani Ulaya hivyo ataonekana tena kwenye benchi katika mchezo wa hatua ya mtoano itakayoanza mwaka 2011.
UEFA wamefikia maamuzi hayo baada ya José Mário dos Santos Félix Mourinho kuwasilisha rufaa yake iliyopinga adhabu aliyopewa ambayo ilikanusha kujihusisha na tuhuma zilizopelekea kutozwa faini sambamba na kufungiwa michezo miwili.
Hata hivyo mbali na kupunguziwa adhabu José Mário dos Santos Félix Mourinho bado analazimika kulipa faini ya paund 33,500 kama alivyoagizwa UEFA kufanya hivyo.
Mourinho alikutwa na mkasa wa kuadhibiwa na UEFA baada ya kuonekana katika picha za televisheni akitoa vishawishi kwa wachezaji wake Xabi Alonso pamoja na Sergio Ramos kufanya makosa kwa makusudi ili waonyeshwe kadi nyekundu kwenye mchezo dhidi ya Ajax uliochezwa Novemba 23 mwaka huu huko Amsterdam Arena.
No comments:
Post a Comment