
Nahodha na beki wa zamani wa timu ya taifa ya Ufaransa Marcel Desailly ametangaza kujiondoa kwenye kinyang’anyiro cha ukocha wa timu ya taifa ya nchi hiyo ambacho kilikuwa kiwashirikisha makocha watano toka sehemu mbali mbali duniani.
Marcel Desailly ametangaza kujiondoa katika kinyang’anyiro hicho kufuatia kuchukizwa na taratibu zinazochukuliwa na viongozi wa chama cha soka nchini Ghana ambapo amedia wamekua hawamjulishi lolote linaloendelea katika hatua zilizosalia kabla ya kutangazwa mshindi wa nafasi ya ukocha mkuu.
Amesema viongozi wa GFA walistahili kumfahamisha kila hatua lakini kumekuwa hakuna lolote linaloendelea hali ambayo anahisi huenda ikawa na njama tofauti ambazo yeye hazijui hivyo ameona ni bora akae pembeni.
Hata hivyo Marcel Desailly ambae alikua mmoja wa wachezaji walioiwezesha nchi ya Ufaransa kuwa bingwa wa dunia mwaka 1998, ameleeza wazi kwamba alitangaza kuwania nafasi ya kocha mkuu wa Black Stars kwa mapenzi yake binafsi na hakushurutishwa na mtu hivyo kujiondoa kwake hakuhusiana na yoyote yule.
Kujiondoa kwa Desailly mwenye umri wa miaka 42 katika kinyang;anyiro hicho, kunawafanya makocha watatu kusalia katika ushindani wa kuwania nafasi iliyoachwa wazi na Mserbia Milovan Rajevac.
Makocha waliosalia katika kinyang’anyiro hicho ni Mserbian Goran Stevanovic, Humberto Coelho pamoja na Herbert Addo huku Can Vanli jina lake likiondolewa katika orodha hiyo kabla ya maamuzi yaliyofikiwa na Marcel Desailly.
No comments:
Post a Comment