
Baada ya kutimiza lengo la kumaliza kwenye nafasi ya kwanza katika msimamo wa kundi A la michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya, meneja wa klabu ya Tottenham Harry Redknapp emesisitiza kuendelea kutumia mfumo wa kushambulia zaidi kwenye michuano hiyo.
Harry Redknapp ametoa msisitizo huo baada ya kuridhishwa na uchezaji wa kikosi chake ambacho kimemaliza michezo ya hatua ya makundi kikiwa kimekwamisha mipira nyavuni mara 18 kwenye michezo sita waliyocheza.
Amesema mfumo huo daima hatosita kuendelea nao na imani utamsaidia katika hatua ya 16 bora huku akitarajia kukutana na klabu yenye uzoefu na michuano hiyo mbali na kikosi chake ambacho kimeshiriki kwa mara ya kwanza msimu huu.
Licha ya kusisitiza kuendelea na mfumo wa kushambulia, meneja huyo wa kiingereza amekiri hatua ya makundi iliyomalizika jana kwa upande wao ilikua ngumu hasa ikizinghatia kundi A lilikua na klabu zenye uzoefu kama Inter Milan, Weder Bremen pamoja na Fc Twenty.
No comments:
Post a Comment