
Shirikisho la soka la Equatorial Guinea limeingia mkataba na aliekua kocha mkuu wa timu ya taifa ya Ivory Coast Henri Michel ambae atakua na majukumu ya kukinoa kikosi cha nchi hiyo kuanzia sasa.
Kazi kubwa ya kocha huyo wa kimataifa toka nchini Ufaransa aliyopewa ni kuhakikisha kikiso cha Equatorial Guinea kinacheza katika kiwango cha hali ya juu ambacho kitaiwezesha timu hiyo kutimiza malengo ya kufanya vyema kwenye fainali za mataifa ya Afrika za mwaka 2012 ambapo nchi hiyo itakua mwenyeji kwa kushirikiana na nchi ya Gabon.
Henri Michel anaichukua timu ya taifa ya Equatorial Guinea huku akiwa na uzoefu wa mazingira ya barani Afrika kwa miaka 15 ambayo imeshuhudia akivinoa vikosi vya nchi kama Cameroon, Morocco, Tunisia pamoja na Ivory Coast.
Katika kinyang’anyiro cha nafasi ya ukocha wa timu ya taifa ya Equatorial Guinea , jina mfaransa Philippe Troussier lilikuwepo lakini kocha huyo ameshindwana na uongozi wa shirikisho la soka la nchi humo kufuatia kuhitaji gharama kubwa za malipo.
No comments:
Post a Comment