KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Saturday, December 11, 2010

UBINGWA WA UINGEREZA BADO KITENDAWILI.


Meneja wa klabu ya Man City Roberto Mancini amesema anaamini kwa sasa ni vigumu kumtabiri bingwa wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza kufuatia uwiyano wa kipoint kutokua mkubwa kati ya vilabu vilivyo kwenye nafasi za juu kwenye msimamo wa ligi hiyo.

Roberto Mancini amezungumzi imani yake juu ya upinzani uliopo kwa sasa huku akieleza wazi kwamba msimu huu umekua mgumu kwa vilabu kama Arsenal, Manchester United pamoja na Chelsea kufikia malengo ya kuongoza ligi kwa point nyingi zaidi ya mengine kutokana na ushindani uliopo.

Amesema hata hivyo huenda upinzani huo umeongezeka kufuatia kila klabu hizo tatu kuonyesha umahiri na umakini mkubwa wakati wa michezo ya makundi ya ligi ya mabingwa iliyomalizika kati kati ya juma hili hivyo katika kipindi hiki michuano hiyo ya Ulaya ikiwa imesimama kila klabu itakua na mtazamo tofauti wa kutaka kuongeza point zaidi.

Mancini amesema anaamini hatua ya mtoano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya itakapoanza mwezi Februari mwaka 2011 ukweli wa nani atakua akiiukaribia ubingwa utafahamika hivyo amewataka mashabiki kutulia na kuona ni yupi atafikia malengo hayo.

No comments:

Post a Comment