KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Saturday, December 11, 2010

WAZIRI WA MICHEZO WA GHANA ATOA KAULI.


Wakati FIFA wakitarajia kutoa kauli juu ya sakata la serikali ya nchini Ghana kuingilia masuala ya soka nchini humo, waziri wa michezo nchini Ghana Akua Sena Dansua ameibuka na kudai serikali haiingilii msuala ya soka.

Akua Sena Dansua ameibuka huku zikiwa simesalia saa kadhaa kabla ya FIFA haijatoa kauli rasmi juu ya nchi hiyo ambayo juzi iligubikwa na skendo za maafisa wa taasisi ya kupambana na kuzuia rushwa kuvamia ofisi za chama cha soka GFA.

Waziri huyo wa michezo nchini Ghana amesema taasisi hiyo haina mahusiano yoyote na serikali ya nchini humo bali ni taasisi inayojitegemea hivyo FIFA wanatakiwa kutoa maamuzi yaliyo sahihi na yenye busara zaidi.

Hata hivyo ameendelea kudai kwamba kulikua hakuna chokochoko zozote kutoka serikalini zilizopelekea maafisa wa taasisi hiyo kwenda kuvamia ofisi za GFA kama ilivyoelezwa siku ya tukia kupitia vyombo mbali mbali vya habari.

Kauli hiyo ya waziri Akua Sena Dansua inaokena kukinzana na maelezo yaliyotolewa na mkuu wa taasisi ya kupambana na kuzuia rushwa alipohojiwa ni wapi wapipopata ruhusa ya kuzikagua ofisi za GFA ambapo alijibu mahakama kuu ya nchini Ghana ndio ilitoa ruhusa, hivyo moja kwa moja inajionyesha dhahiri serikali imehusika.

Tayari hofu imetanda miongoni mwa viongozi wa serikali pamoja na wadau wa soka nchini Ghana ya kuhisi huenda FIFA wakatoa kauli ya kuifungia nchi hiyo kujishughulisha na masuala la soka la kimataifa hadi hapo itakaporekebisha kasoro zilizopo kati ya viongozi wa serikali dhidi ya viongozi wa GFA.

No comments:

Post a Comment