KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, December 2, 2010

Ian Holloway AWASUBIRI KWA HAMU MAN UTD.


Meneja wa klabu ya Blackpool Ian Holloway ametamba kuibanjua Man Utd mwishoni mwa juma hili pale kikosi chake kitakapokua nyumbani huklo Bloomfield Road kikicheza mchezo wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza.

Ian Holloway ametoa tambo hizo, huku akikiri kuchagizwa na ushindi wa mabao manne kwa sifuri ulioipa nafasi klabu ya West Ham Utd kutinga kwenye hatua ya nusu fainali ya kombe la ligi na kuivua ubingwa Manchester United.

Amesema katika soka hakuna linalo shindikana hivyo anaamini kikosi chake mwishoni mwa juma hili kitafungua ukurasa mpya wa historia kwa kuinyuka Man utd ambayo mpaka sasa bado haijapoteza mchezo hata mmoja wa ligi licha ya kufungwa na wagonga nyundo wa London West Ham usiku wa kuamkia jana kwenye michuano ya kombe la ligi.

Ian Holloway ametamba kuifahamu uzuri klabu hiyo inayonolewa na babu Alex Ferguson huku akithibitisha kuyabaini makosa ambayo atayatumia kama sehemu ya kuukata mzizi wa kuhakikisha Man Utd wanapoteza point tatu kwa mara ya kwanza.

No comments:

Post a Comment