
Hatimae shirikisho la soka nchini Nigeria limeingia mkataba wa miaka minne na Samson Siasia alieshinda kinyang’anyiro cha kukinoa kikosi cha timu ya taifa ya nchi hiyo Super Eagles mwezi uliopita.
NFF wameingia mkataba na mshambuliaji huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Nigeria katika makao makuu ya ofisi za shirikisho hilo zilizopo mjini, Abuja huku makubaliano yakimtaka Samson Siasia kuhakiksiha anafikai malengo yaliyowekwa ndani ya miaka miwili ijayo.
Raisi wa shirikisho la soka nchini Nigeria Aminu Maigari amesema makubaliano hayo ya miaka miwiwli ijayo ni kuhakikisha kocha huyo anaiwezesha timu ya taifa ya Nigeria kushiriki fainali za mataifa ya bara la Afrika ambapo kwa sasa mataifa mbali mbali ya bara hilo yapo kwenye mchakato wa kusaka nafasi.
Aminu Maigari ametoa sababu za kumtaka Samson Siasia kuhakikisha anafanya hivyo, ni kufuatia soka la nchini Nigeria kuporomoka kwa kiasi kikubwa hadi kufikia hatua ya kushindwa kupata mafanikio waliyoyapata miaka ya nyuma ambayo kwa mara ya mwisho nchi hiyo ilifanikiwa kutwaa ubingwa wa bara la Afrika mwaka 1994.
Hata hivyo raisi huyo wa NFF amesema wanamuamini Samson Siasia ataweza kufanya kazi hiyo na kufikia malengo hivyo amewataka viongozi wenzake pamoja na wadau wa soka nchini Nigeria kumpa ushirikiano wa kutosha.
Itakumbukwa kuwa Samson Siasia alikuwa akiiwani nafasi ya kuinoa timu ya taifa ya Nigeria sambamba na Stephen Okechukwu Keshi ambae alijumuika nae kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Nigeria miaka ya 90 na kufanikiwa kutwaa ubingwa wa bara la Afrika.
No comments:
Post a Comment