
Meneja wa klabu ya Stoke City Tony Pulis ameweka hadharani mipango yake ya usajili kupitia dirisha dogo litakalofunguliwa mwanzoni mwa mwezi Januari na kufungwa mwishoni mwa mwezi huo mwaka 2010.
Mikakati ya Tony Pulis katika usajili wa dirisha dogo imemlenga mchezaji mmoja tu, na huyu si mwingine ni Jermaine Pennant ambae kwa sasa anaichezea Stoke City kwa mkopo akitokea Real Zaragoza ya nchini Hispania.
Amesema mikakati yake ni kuhakikisha winga huyo wa kiingereza anamsajili moja kwa mopja baada ya kuridhishwa na kiwango chake na tayari uongozi wa klabu ya Real Zaragoza umeshatangaza kuhitaji kiasi cha paund million 6 kama ada ya uhamisho wake.
Hata hivyo Tony Pulis amekiri kuwepo kwa ugumu wa mkakati huo ambao anahisi huenda ukakwamishwa na uongozi wake ambao mpaka sasa umeshindwa kumthibitishia kama inawezekana kukamilisha dili la kumsajili moja kwa moja winga huyo mwenye umri wa miaka 27.
No comments:
Post a Comment