


Meneja wa klabu ya Liverpool Roy Hodgson amekanusha taarifa za klabu hiyo kuwa mbioni kutumia dirisha dogo la usajili kwa kumpata kiungo wa kimataifa toka nchini Brazil Ronaldinho Gaucho, winga wa kimataifa toka nchini Uingereza Ashley Young pamoja na mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Uruguay Luis Suarez.
Roy Hodgson amelazimika kukanusha taarifa hizo kufuatia uvumi uliotanda katika kila kona ya dunia hii ambapo mabingwa hao wa zamani wa nchini Uingereza yasemekana wanataka kujiimarisha zaidi kufuatia mikakati iliyowekwa na wamiliki wapya wa klabu hiyo.
Mzee huyo mwenye umri wa miaka 63 amekiri ni kweli watafanya usajili kupitia dirisha dogo mwezi januari mwaka 2011, lakini si kwa wachezaji hao ambao amesema yeye binafsi anawakubali kwa shughuli wanayoifanya wanapokua uwanjani.
Amesema hakuwahi kuwasilisha jina na mchezaji yoyote kati ya wachezaji hao wa tatu katika meza ya wakurugenzi wake na amekua akishangazwa na taarifa zinazotolewa juu ya wachezaji hao watatu.
No comments:
Post a Comment