KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, December 2, 2010

MASHABIKI WA ASTON VILLA WATIWA NGUVUNI.


Jeshi la polisi mjini Birmingham linawashikilia watu saba kwa makosa ya kujihusisha na fujo zilizojitikeza kwenye mchezo wa hatua ya robo fainali wa michuano ya kombe la ligi uliochezwa usiku wa kuamkia hii leo ambapo wapinzani wa jadi wa mji huo Birmingham City walikuwa akipapatuana na Aston Villa.

Taarifa zilizotolewa na jeshi hilo la polisi kupitia kituo cha West Midlands zimeeleza kuwa watu hao saba wanaoshikiliwa kwa hivi sasa walionekana kuwa chanzo cha zogo zililojitokeza mara baadaya mchezo huo kumalizika kupitia picha za televisheni.

Taarifa hizo pia zimeleeza kuwa, imebainika kuwa watu hao saba ni mashabiki wa klabu ya Aston Villa ambao walishikwa na hasira baada ya kufungwa na wapinzani wao mabao mawili kwa moja na kikosi chao kutupwa nje ya michuano ya kombe la ligi.

Mashabiki hao walinaswa na camera za nje ya uwanja ambapo walionekana wakitupa mawe kwenye vioo vya jingo la uwanja wa St Andrews hatua mbayo ilisababisha kuanza kugombana na mashabiki wa klabu ya Birmingham City.

Katika hatua nyingine mashabiki wa klabu ya Birmingham City waliingia uwanjani mara baada ya kipenga cha mwisho kupulizwa kitendo ambacho kimetafsiriwa kwama furaha kwao kufuatia klabu hiyo kutinga kwenye hatua ya nusu fainali ya kombe la ligi.

Hata hivyo hatua hiyo imeonekana kumuweka njia panda meneja wa klabu hiyo Alex McLeish ambapo alionyesha kuhofia huenda Uingereza ikashindwa kupewa kura za kutosha ambazo zitaiwezesha kuandaa fainali za kombe la dunia za mwaka 2018, lakini baadae alijisahisha mwenyewe kwa kusema anaamini suala hilo haliwezi kuwa kigezo cha kuikwamisha nchi hiyo kupata nafasi hiyo muhimu.

Alex McLeish pia akazungumzia mchezo wa jana ambapo amesema kwa ujumla kikosi chake kilicheza kwa kujituma na kuonyesha malengo ya kusaka ushindi ambayo yalitimia katika dakika za lala salama.

No comments:

Post a Comment