




Wakati asilimia kubwa ya mashabiki wa soka ulimwenguni kote wakijiuliza nini kilichoisibu Uingereza hadi kufikia hatua ya kushindwa kupata nafasi ya kuwa mwenyeji wa fainali za kombe la dunia za mwaka 2018, sababu muhimu ya nchi hiyo kushindwa zimetolewa.
Sababu kubwa ambayo imeifanya Uingereza kubwagwa katika kinyang’anyiro hicho ni maamuzi ya wajumbe wa kamati kuu ya FIFA ambao jana walikutana mjini Zurich nchini Uswiz na kukamilisha zoezi la kupiga kura ambalo liliamua nchi ya Urusi kuwa mwenyeji wa fainali hizo.
Matokeo ya zoezi hilo la upigaji wa kura yameonyesha kuwa Uingereza ilikua haijiwezi kwa hali yoyote baada ya kutupwa vibaya na kinara Urusi kufuatia kupata kura mbili katika mzunguuko wa kwanza
Katika mzunguko wa kwanza.
Uingereza 2 (Wakaenguliwa), Uholanzi -Ubelgiji 4; Hispania-Ureno 7 na Urusi 9
Katika mzunguko wa pili.
Uholanzi -Ubelgiji 2; Hispania-Ureno 7; Urusi 13 (Urusi wakashinda)
Katika kura za kuwania kinyang’anyiro cha kuwa mwenyeji wa fainali za mwaka 2022
Mzunguuko wa kwanza: Australia 1 (Wakaenguliwa); Japan 3; Marekani 3; Korea Kusini 4 na Qatar 11
Mzunguuko wa pili: Japan 2 (Wakaenguliwa); Korea Kusini 5; Marekani 5 na Qatar 10
Mzunguukio wa tatu: Korea kusini 5 (Wakaenguliwa); Marekani 6 na Qatar 11
Mazunguuko wa nne: Marekani 8 na Qatar 14 wakatangazwa kuwa washindi.
No comments:
Post a Comment